Priscilla Sitienei: 'Mwanafunzi mwenye umri mkubwa zaidi wa shule ya msingi duniani' afariki akiwa na umri wa miaka 99 nchini Kenya

Mwanamke mwenye umri wa miaka 99, anayeaminika kuwa mwanafunzi mwenye umri mkubwa zaidi wa shule ya msingi duniani, amefariki dunia kwa amani nyumbani kwake nchini Kenya, mjukuu wake ameiambia BBC.

Priscilla Sitienei alianza kupata matatizo ya kiafya baada ya kuhudhuria darasani siku ya Jumatano.

Yeye, na wanafunzi wenzake wenye umri wa miaka 12, walikuwa wamejitayarisha kwa ajili ya mitihani ya mwisho iliyopangwa kuanza wiki ijayo.

Hadithi ya Bi Sitienei ilihamasisha filamu na sifa kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la utamaduni na elimu, Unesco.

Alikulia katika nchi ya Kenya iliyokuwa inamilikiwa na Waingereza na aliishi katika harakati za kupigania uhuru wa nchi yake.Aliiambia Unesco mwaka jana kuwa alitaka kuwahamasisha akina mama vijana kurejea shuleni.

"Nilitaka kuonyesha mfano sio kwao tu bali kwa wasichana wengine ulimwenguni ambao hawako shuleni, bila elimu, hakutakuwa na tofauti kati yako na kuku," alisema.

Alijiunga na Shule ya Maandalizi ya Leaders Vision mwaka wa 2010, lakini pia alihudumia kijiji chake cha Ndalat katika Bonde la Ufa kama mkunga kwa zaidi ya miaka 65.

Anayejulikana kwa upendo kama "Gogo", ambayo ina maana ya nyanya katika lugha ya Kikalenjin, aliiambia BBC mwaka wa 2015 kwamba hatimaye alikuwa akijifunza kusoma na kuandika - fursa ambayo hakuwahi kupata kama mtoto.

Mara nyingi alikabiliana na watoto ambao hawakuwa shuleni na kuwauliza kwa nini.

"Wananiambia kuwa ni wazee sana," alisema. "Ninawaambia: 'Sawa niko shuleni na ninyi pia mnapaswa.'

"Ninaona watoto ambao wamepotea, watoto ambao hawana baba, wanazunguka tu, hawana matumaini. Nataka kuwatia moyo kwenda shule," aliongeza.

'Ujumbe wake unaendelea'

Mwanzoni shule ilimkataa lakini punde ikaelewa jinsi alivyojitolea kujifunza.

Hadithi yake ilisimuliwa katika filamu ya Kifaransa iliyoitwa Gogo, ambayo ilimfungulia fursa ya kutembelea Ufaransa na kukutana na mke wa rais Brigitte Macron.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Nepali Graphics - Learn design, Animation, and Progrmming