Mudryk: Mfahamu mchezaji mpya wa Chelsea mwenye ndoto ya kushinda taji la Ballon d'Or



Chelsea wametumia kitita cha pauni milioni 62 kumnunua mchezaji mwenye mabao 12 katika maisha yake ya soka ambaye hajawahi kucheza nje ya Ukraine, je Mykhailo Mudryk ni nani na kwanini amemvutia macho mengi?

 

Winga wa kushoto wa Shakhtar Donetsk, 22, ambaye ameichezea Ukraine mara nane, aliimarisha nyota yake  katika Ligi ya Mabingwa msimu huu


Hadi kufikia msimu huu alikuwa amefunga mabao mawili pekee katika mechi 47 alizochezea klabu tatu tofauti za nchi yake.

 

Lakini msimu huu uwezo wake na wasifu wake umepanda juu zaidi.

 

Chelsea wamemsajili Mudryk kwa mkataba wa euro 100m

Mudryk alifunga mara tatu katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa akiichezea Shakhtar - huko Leipzig na kisha magoli mawili dhidi ya Celtic - licha ya kuondolewa kwao. Hiyo ni zaidi ya mchezaji yeyote wa Chelsea anayesimamiwa.

 

Pia alitengeneza pasi mbili za mabao, zaidi na wachezaji wenzake wa hivi karibuni wa Blues.

 

Mudryk, ambaye ametia saini kandarasi hadi 2031 na anaweza kuigharimu Chelsea pauni milioni 27 zaidi za bonasi, amefunga mabao saba katika mechi zake nane za mwisho za Ligi Kuu ya Ukraine, huku akitoa usaidizi wa magoli sita katika mechi 12.

 

Kwa kweli amekuwa na wastani wa bao au asisti kila dakika 65 kwenye ligi ya Ukraine msimu huu, na kila dakika 79 msimu uliopita.

 

Haya yote huku kukiwa na kutokuwa na uhakika katika nchi yake na uvamizi unaoendelea wa Urusi. Msimu huu, Shakhtar wamecheza mechi za nyumbani huko Kyiv, Lviv na mji mkuu wa Poland Warsaw.


Mudryk hakosi tamaa na alizungumzia nia yake ya kushinda taji la Ballon d'Or wikendi hii.

 

Akikabidhiwa kombe la mchezaji bora wa mwaka wa Shakhtar kwa mara ya pili mfululizo, aliambia tovuti ya klabu yao: "Hakuna aliyetarajia ningeshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Shakhtar mnamo 2021 na hakuna anayetarajia nipate hata ule mpira wa Dhahabu pia, lakini inaweza kutokea siku moja. Hili ni moja ya malengo yangu binafsi."

 

Mudryk amecheza mechi nyingi zaidi kwa Roberto de Zerbi, ambaye alikuwa bosi wa Shakhtar mnamo 2021-22, kuliko meneja mwingine yeyote.

 

Muitaliano huyo, ambaye sasa anaiongoza Brighton, alisema hivi majuzi: "Nafikiri Mudryk anaweza kushinda Ballon d'Or siku zijazo."

 

Mudryk alipanda daraja baada ya wachezaji wengi wa kigeni wa Shakhtar kuondoka bila malipo kufuatia uamuzi wa Fifa mwaka jana kwamba watu wasio raia wa Ukraine wanaweza kusimamisha kandarasi zao kufuatia uvamizi wa Urusi.

 

Shakhtar ilidai fidia ya pauni milioni 43 kutoka kwa Fifa kutokana na kupoteza ada ya uhamisho - na pengine ilisababisha klabu hiyo kudai ada kubwa kama hiyo kwa moja ya mali zao chache zinazoweza kuuzwa.

 

Hadi msimu huu Mudryk hangejulikana sana nje ya nchi yake.

 

Alikuwa na muda wa mkopo wa kufunga goli akiichezea  Arsenal Kyiv mnamo 2018-19 na Desna Chernihiv mnamo 2020-21, na pia mechi nyingi za ya nyumbani bila kucheka na wavu.

 

Alianza kwa mara ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita na kufunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu ya Ukraine ambayo haikumalizika kwa sababu ya vita.

 

Lakini imekuwa mchezo wake msimu huu ambapo Mudryk alijifanya kuwa shabaha ya timu kadhaa za juu za Uropa.

 

Rais wa Shakhtar Rinat Akhmetov alisema: "Nina uhakika kwamba Mykhailo atashinda heshima, huruma na upendo wa wajuzi wote wa soka la dunia kwa kasi yake, mbinu yake, uchezaji wake wa kuvutia na mzuri."

 

Mudryk pia amekuwa mchezaji wa kawaida katika timu ya Ukraine tangu alipocheza kwa mara ya kwanza mnamo Juni 2022, na mechi sita kati ya nane alizocheza dhidi ya Scotland, Wales na Jamhuri ya Ireland.

 

Chelsea ilimwita Mudryk "mchezaji stadi na mwenye kasi nyingi" na "mmoja wa wachezaji hatari sana washambuliaji barani Ulaya katika hali ya ‘’mmoja kwa mmoja ".

 

Mwenyekiti wa Blues Todd Boehly na mmiliki mwenza Behdad Eghbali waliongeza katika taarifa: "Ni kipaji cha kusisimua sana ambaye tunaamini atakuwa nyongeza nzuri kwenye kikosi chetu sasa na katika miaka ijayo."

 

Post a Comment

Previous Post Next Post

Nepali Graphics - Learn design, Animation, and Progrmming