-->    

Rais wa DR Congo aishutumu Rwanda juu ya usalama wa nchini mwake

 


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi ameishutumu Rwanda kuwa chanzo cha kukosekana kwa utulivu katika eneo hilo, katika kujibu vikali maoni ya waziri wa baraza la mawaziri wa Rwanda Claire Akamanzi katika Kongamano la Kiuchumi la Dunia huko Davos.


"Samahani, suala la ukosefu wa usalama tulilonalo katika eneo la Maziwa Makuu linaitwa Rwanda," alisema. Bw Tshisekedi aliongeza kuwa "Rwanda inawaunga mkono waasi wa M23" ili kuleta ukosefu wa usalama mashariki mwa DR Congo - madai ambayo Rwanda imekanusha.


Aliwashutumu waasi kwa kuua zaidi ya raia 100 huko Kishishe ili "kuitisha" jamii kutoka katika kijiji hicho, ambacho kina "madini ya thamani ".


Bw Tshisekedi pia alisema M23 imekuwa haiheshimu makubaliano ya amani, ambayo yaliwataka waasi kuondoka mara moja kutoka katika maeneo waliyoteka.


"M23 bado ipo, wanajifanya kama wanahama lakini wapo tu, wanazunguka tu na kupelekwa mahali pengine, na wanakaa katika miji ambayo wameiteka," alisema.


Akizungumza katika kikao cha WEF siku ya Jumanne, Bi Akamanzi alimwambia Bw Tshisekedi kwamba "ikiwa usalama ni tatizo kubwa kwako, na ni wazi kama ungeweza kulitatua kama serikali ya DRC au jeshi la DRC, ungekuwa umelimaliza kufikia sasa".


"Ninaamini suluhu liko mikononi mwako kumiliki tatizo lakini [pia] kufanya kazi na wale ambao wanaweza kulitatua... kwa sababu usalama ni muhimu kwa uwekezaji," Bi Akamanzi aliongeza.


Soma zaidi:


Kwanini hali ya usalama imeendelea kuwa tete nchini DRC?

Rwanda yapinga shutuma kuwa ilishambulia vikosi vya DRC

Techy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ART
Techy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ARTTechy Pranav PKD ART