Mtoto miongoni mwa watu sita wa familia moja waliouawa California Marekani


 Vizazi vinne vya familia moja viliuawa katika kile kinachotajwa kama ‘mauaji ya magenge ya makundi ya uuzaji wa dawa za kulevya’ katika makazi ya California yanayojulikana na polisi kwa shughuli zinazohusiana na dawa za kulevya.

Mama mwenye umri wa miaka 16, mtoto wake wa kiume wa miezi 10 na nyanya mtoto walikuwa miongoni mwa wahasiriwa, polisi na familia wanasema.

Nyumba hiyo iliyoko Goshen, yenye wakazi 3,000, ilikuwa imevamiwa na polisi wiki iliyopita.

Polisi wanasema wanawasaka washukiwa wawili wanaojulikana katika "mauaji yaliyolengwa".

Katika kikao na wanahabari siku ya Jumanne, Sherifu wa Kaunti ya Tulare Mike Boudreaux hakutaja majina ya washukiwa hao, akisema kuwa ni kutokana na uwezekano kwamba wauaji walikuwa wakiangalia ili kuepuka kukamatwa, lakini akafichua kuwa mengi tayari yanajulikana kwa mamlaka kuwahusu.

Watu hao sita waliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatatu. Watu watatu walinusurika.

"Hakuna hata moja kati ya haya lililotokea kwa bahati mbaya," Bw Boudreaux alisema. "Ilikuwa makusudi, na ya kutisha."

Wahasiriwa wametambuliwa na wachunguzi kama:

  • Rosa Parraz, 72
  • Eladio Parraz Jr, 52
  • Jennifer Analla, 50
  • Marcos Parraz, 19
  • Elyssa Parraz, 16
  • Nycholas Parraz, umri wa miezi 10

Kulingana na Bw Boudreaux, mtu mmoja aliyenusurika alilala sakafuni, miguu yake ikiwa juu ya mlango ili kuwazuia washambuliaji kuingia ndani ya chumba hicho.



Post a Comment

Previous Post Next Post

Nepali Graphics - Learn design, Animation, and Progrmming