Je Urusi inataka mamlaka ya kusambaratisha mataifa mengine?


 Rais Zelensky alikuwa na ujumbe wa wazi - akiwashukuru washirika wa Magharibi kwa msaada ambao wametoa hadi sasa katika vita ya taifa lake dhidi ya Urusi, lakini aliweka wazi Ukraine inataka msaada zaidi wa kijeshi na wa haraka.

Rais huyo alizungumza mengi kuhusu muda, akionya "Urusi inataka mamlaka ya kuharibu mataifa", na akisisitiza "Kremlin lazima ishindwe".

Zelensky ambaye anazungumza wakati huu kwenye mkutano na mataifa zaidi 50 yanayojiandaa kuisaidia Ukraine kwa silaha. Mkutano huo unafanyika nchini Ujerumani.

Alisisitiza kuwa hakuna muda mwingi. Ni wazi kwamba kumekuwa na kiwango kikubwa cha umakini katika suala la vifaru vya vita, na watu wengi wanatazama kuona nini Waziri mpya wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, anasema katika mkutano huu.

Pia tulisikia kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akizungumzia kwamba huu ni wakati muhimu kwa Ukraine.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Nepali Graphics - Learn design, Animation, and Progrmming